Monday, January 25, 2016

MY IN FORMATION

 Mimi ni abdul-rahim Salum Suleiman.nimezaliwa tarehe, 04/11/1987 katika hospitali ya Abdalla Mzee mkoani kusini Pemba.
no
mimi ni mtoto wa sita (6) wa mzee salum suleiman khamis(Sahera) kati ya watoto kumi na sita(16) wakiwa wanawake kumi na wanaume sita.lakini pia ni mtoto wa tatu (3) wa Bi Nafuu Bakar Maalim kati ya  watoto nane(8)wakiwa wanawake watano(5) na wanaume watatu(3).nimeanza kusoma katika skuli ya msingi darasa la kwanza mwaka 1995 katika skuli ya kilindi na nilimaliza masomo yandu ya msingi mwaka 2002. hapo nilijiunga na sekondari katika skuli ya sekondari ya kilindi mwaka 2003 nilipaata kusoma shule mbali mbali za sekondari ikiwemo skuli ya sekondari fidal castro na haile selassie mjini zanzibar. nilimaliza masomo yangu ya sekondari ya awali (kidato cha nne) mwaka2008. pia niliendelea na sekondari ya juu (kidato cha sita) katika skuli ya sekondari ya Tumekuja mwaka 2009 na nilimaliza mwaka 2011.
nilijiunga na masomo ya stash hada (diploma) ya utunzaji wa kumbukumbu (diploma in records and archives management katika Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar mwaka 2012 na nilimaliza mwaka 2013.
kutokana na maisha yangu kua magumu sana wazazi walishindwa kunisomesha baada ya kufeli masomo yangu ya mara ya kwanza kidato cha pili mwaka 2005 katika skuli ya kilindi chake chake Pemba. hapo niliamua kujisomesha mwenyewe kuazia kidato cha tatu mpaka kufikiastash hada ijapo nilikua nikipata baadhi ya msaada wao wakati wakimasomo.
utakua unajiuliza nilijisomeshaje?
Wakati nilipo kua najisomesha nitambua kua mimi ni mtoto wa kimaskini napaswa nijitahidi kutafuta ada ya masomo lakini ppia kufanya vizuri katika masomo yangu.kwahivyo niliamua kufanya kazi mbali mbali ambazo zilisaidia kuingiza kipato katika maisha yangu ijapo kua hakikua kinatosheleza.nilijaribu kujifunza ufundi wa nyumba kupiga plasta na pia kupiga dari pamoja na kujenga paa. nilipo ona harakati hizi zilikua ngumu kulingana na mda wa shule niliamua kujitupa katika harakati za ulinzi katika sehemu za maduka,majumba,mahotelini na katika sehemu za makampuni.
namshukuru mungu nilisoma na nilimaliza kwa kupitia harkati hizi baada ya hapo niliamua kutafuta ajira ya serikali lakini pia haikua bahati yangu kupata ajira hio.
kutokana na hali hio niliamua kujiunga na shahada ya elimu katika vyuo vikuu vya Tanzania ambapo nilianzia na chuo kikuu cha Tumaini mwaka 2014/15. Lakini kutokana na ada yake kua kubwa na kukosa udhamini wa serikali nilishindwa kuendelea na chuo hicho.hivyo kwa mwaka uliofata nilihamia chuo kikuu cha Taifa Zanzibar